Jumamosi, 3 Agosti 2013

MKE WA MTU NI SUMU



FUMANIZI  ZITO
Jamaa mmoja  akumbwa na fumanizi la ajabu katika moja kati ya lorge mashuhuli hapa mjini iitwayo mchana lorge. Ni mchongo uliofanywa na mpenzi wa zamani wa mwaume huyo baada ya kumkacha, akaamua kumsambazia noma kwa kumvujishia mume wa mwanamke husika ambaye alikuwa akitoka na mwanaume huyo baada ya kumsaliti, jamaa huyo jina(………..) limehifadhiwa ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu mashuhuri hapa  Tanzania anaonekana kuwa na soni kubwa baada ya kukutwa live na mume wa mwanamke huyo ambaye alikuwa akideti naye. Ilikuwa ni muda wa jioni fulani hivi ambapo wahusika walikuwa wakijiachia kwa starehe zao baada ya kuamini kuwa wapo pekeyao ndani ya lorge hiyo, bila kujua chochote katikati ya mchezo mlango ukafunguliwa kwa nguvu kubwa paaa…………….. Mume wa mwanamke yupo ndani na shahidi wake ambaye ni mpenzi wa zamani wa mwanaume aliye fumaniwa, kwa aibu na woga wa ajabu mwanaume akawa hajui nini la kufanya ili kujinusuru na dhahama iliyomkuta pale lorge, akasema bro….. nisam….!!!!!!!!!!! Ni shetani tuuu ndiye aliye nikumba. Kwa bahati mbaya zaidi mume wa mwanamke huyo alifanikiwa kuchukua nguo zote za wahusika hao kisha akawapa jukumu la kuchagua adhabu kwa wote wawili  na machaguo yalikuwa kama yafuatayo  kuuawa, kweenda polisi wakiwa kama walivyo zaliwa, kupigwa picha na kupelekwa kwenye vyombo vya habari, na mwishowe ilikuwa kuwatembeza wakiwa kama jinsi walivyozaliwa kutoka kwa mama zao!!!!!!!!!!!!!! Kutoka eneo la tukio na kuelekea viwanja vya michezo . JAMANI WATANZANIA MAISHA YA KUTEMBEA NA WAKE ZA WATU SI VYEMA KWANI AIBU KAMA HII NI HATARI KUBWA SANA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni