Jumamosi, 3 Agosti 2013

TAARIFA KUTOKA TCU KWA MWAKA WA MASOMO 2013/2014



Wapenzi wasomi watarajiwa wa elimu ya juu mnatakiwa kuangalia majina yenu yaliyotolewa na TCU kwani kuna baadhi ya watahiniwa takribani elfu nane na miatano hawajafanikiwa kuchaguliwa kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali vya hapa nchini kutokana na sababu tofauti tofauti   ikwemo na kukosea baadhi ya kanuni za uombaji pamoja na kukosea jinsi ya uandishi wa majina husika ya waombaji. Hivyo basi ni vyema kutazama na kuangalia majina hayo kama jina lako halitakuwepo kwenye orodha hiyo basi fahamu kuwa huna tatizo lolote lakini endapo utafanikiwa kuliona jina lako katika orodha hiyo fahamu kuwa unatatizo na linatakiwa kufanyiwa urekebishaji mapema na kwa haraka sana.  TCU wametoa tarehe ya mwisho ya kufanya marekebisho kuwa ni  TAREHE  09/ 08/ 2013 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni