Ijumaa, 26 Julai 2013

SAFARI YA PAMOJA


MAPENZI SAFARI

Mnamo siku ya i

juma  tarehe 12 ya mwezi wa sita wapenz wawili walikuwa katika harakati za kutaka kufanya safari ya pamoja ya kuelekea nyumbani baada ya kufungwa kwa chuo chao cha TEKU. Kwa uchovu wa mitihani ya UE pamoja na swaumu aliyokuwa nayo mmoja wa wapenzi hao wakaamua kuondoka pamoja kwa lengo la kudhihilisha mapenzi yao, walipofika standi kuu ya mabasi ya mikoani wakajaribu kutafuta basi ambalo linaweza kuwabeba wote wawili kwani mmoja kati yao alikuwa anatakiwa kuishia mjini iringa na mwingine anatakiwa kuishia mjini morogoro. Walipofika stand wakaangaika sana kupata usafili wa pamoja na hatimaye walifanikiwa kupata gari la pamoja katika safari yao,  wakakata tikeki katika gari la hood na baadae wakaamua kurudi nyumbani kujiandaa na safari yao. Mapenzi mazito sana!, walipofika nyumbani mpenzi wa kiume  akawa anaburn CD kwa ajili ya mpenzi wake. Katikati ya harakati za maandalizi ya safari yao mpenzi wa kike akaanza kulia kwa undani wa penzi lake kwa mpenzi wake kwa kudai kuwa wasiondoke kwani atapata shida sana kwakua hajazoea kukaa peke yake kwa muda mrefu sana, kwa hali halisi watu hao ni lazima waachane kwa muda huo kwani walikuwa wanakwenda kutimiza wajibu wao wa kufanya field katika shule za sekondari tofauti; kwa kujaribu kuwekana sawa ili mambo yaendelee kuwa vyema iliwalazimu wachelewe kulala mpaka ilipo timu saa sita usiku. Ilipo fika alfajiri ya saa kumi wapenzi hao iliwalazimu  kuamka kwa kujiandaa na safari ya kuelekea iringa pamoja na morogoro, wakajiandaa kwa haraka zaidi na stadi zaidi. M ara ghafla wakapigiwa simu na wale waliowakatia tiketi kwa ajili ya usafili wao na kuwataka wabadilishe gari la kupanda kutoka hood kwenda sumry inayotoka mbeya kwenda dodoma, haikuwa shida kwa wapenzi hawa kukubali kwani tayari walikwisha kata tiketi kwa ajili ya kusafili siku hiyo. Ikawalazimu kujongea mpaka stendi ya mamajohn kwa kusubiri usafili, kwa bahati nzuri sana sumry iliwai kufika na wapenzi hao wakapanda gari hiyo tayari kwa kuaanza safari yao,  safari kwa upande wa watu hawa wawili haikuwa nzuri sana kwani hawakuwa tayari kuachana kirahisi  ila majukumu yaliwafanya waweze kutekeleza jukumu la kuachana katikati ya safari  kama kawaida gari lazima lisimame kwa lengo la kuchimba dawa, hapo magari kadhaa yakakutana na wapenzi hawo wakakutana tena na baadhi ya marafiki zao waliopanda gari jingine. Baada ya muda kidogo gari la wapenzi hao likaondoka katika eneo la tukio na kufika umbali kidogo gari hilo likapata hitirafu na kukaa pembeni kifaa kilicho haribika katika gari hilo ni kikubwa sana kilichofanya gari hilo lishinndwe kuendelea na safariyake, na abilia kutangaziwa kuwa hawanabudi kusubili gari lingine kutoka mbeya mjini lije makambako kwa ajli ya kuwachukua abilia na kuenndelea na safari ya kuelekea Dar es salaam, baada ya kukaa kwa muda mrefu likatolewa tangazo na kondakta wa gari hilo kuwa abilia wanaoishia morogoro wanatakiwa washuke na kupanda gari lingine ambalo ni Alsaedy, kitendo hiki kiliumiza sana nyoyo za wapenzi hao wawilin kwani wawili kwani endapo wangeachana hapon lengo lao lisingetimia la kusafili pamoja mpaka Iringa. Wapenzi hao wakawa wanafuraha lakini yule mwanaume ilimbidi ashuke kwenye Sumry na kutoa mizigo nje ya gari kwa kusubili uamuzi wa utawala wa gari lao la Sumry, baada ya muda kadhaa likafika gari husika yaani Alsaedy kwa lengo la kuwabeba abilia  hapo pia ikatolewa kauli nyingine kuwa abilia ishilini pekee ndio wanaotakiwa kupanda gari hiyo na kuelekea sehemu husika. Wapenzi hao wakafurahi sana na kufanya harahara kupakia mizigo yao kwenye gari lengwa, baada ya kufanikiwa kwa suala hilo furaha ya wapenzi hao ikarudi tena japokuwa haikuwa sawia sana kwakuwa walijua tu kuwa kuna muda utafika wataachana wapenzi hao, basi kwa umbali mrefu wlikuwa wakipia stori za kujiliwaza ihali ya kuwa walijua kuwa hawana muda mrefu  waa kukaapamoja. Safari ilipokuwa ikikaribia iringa wapenzi hao wakaingia tena kwenye dimbwi la huzuni kwani hawakuweza kabisa kujizuia kuonyesaha hisia zao juu ya mapenzi yao! Mwanamke akaanza kulia tena kwa kufosiwa na upendo wa moyo wake juu ya mpenzi wake, baada ya kubembelezwa na mpenziwe hatimaye mwanaume nae akaanza kulia pia kwa kdhihilisha upweke wa muda mrefu kutoka kwa mpenziwe punde tu watakapo achana watu haoo! Kama ilivyo ada gari likafanikliwa kuingia stend ya Iringa na wapenzi hao wakasindikizana mpaka mlangoni mwa gari na kuondoka, kwa upande wa mwanamke akapanda pikipiki tayari kwa kupelekwa nyumbani na kwa upande wa mwanaume akaendelea na safari kuelekea Morogoro.
      Msimamo wa penzi unatokana na wawli wapendanao na si wale wanao waangalia kwani hawanadhabiti yoyote kuhusu mapenzi ya wawili hao. Katika ulimwengu wa sasa kuna vitu vingi sana vinavyo vunja na kuharibu undugu na urafiki lakini  vitu hatari sana kwa suala hili ni Mapenzi na Pesa. Katika mapenzi hakuna wakumwamini katika wale wanaoyaangalia mapenzi yako iwe ndugu, rafiki, jirani na binadamu wengine wote. Kama unaamini unapendwa nawe penda sana  na kana moyo wako unapenda usifiche hisia zako juu ya uumpendaye.
     MAISHA HUJENGWA NA PIA HUARIBIWA NA BINADAMU UMAKINI UNAHITAJIKA KATIKA UTENDAJI  KWANI DAIMA VIVURUGE BADO WAPO HUMUHUMU DUNIANI…………………!!!!!!!!!!!!!!